Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Tuesday, 21 November 2017

Je, Dk.Shika afanya shuting na Dogo janja?

 Kila siku umaarufu wa Dk.Luis Shika unazidi kuongezeka na hata baadhi ya watu na makampuni wameanza kumtumia katika biahara zao, hii ni pamoj na picha zilizoanza kusambaa zikimuonyesha yupo na msanii wa muziki Dogo Janja. 

Kutokana na picha ambazo zimeanza na zinaendelea kusambaa mtandaoni zikimuonyesha Dk.Shika au Mzee wa 900 Itapendeza akiwa katika muonekano wa kipapa na huku akiwa ana kula bata na warembo, jambo linalohisiwa kuwa huwenda kukawa na video mpya ya muziki kutoka kwa msanii Dogo Janja hivyo ametumika kama muhusika mkuu. 

Dk. Luis Shika amejipatia umaarufu kutokana na sakata la kuuzwa kwa nyumba za mfanyabiashara Said Lugumu, ambapo aliingilia katikwa kutaja kiwango kikubwa cha pesa ili aweze kununua nyumba hicho ila cha kushaa baada ya kuibuka mshindi hakuwa na 25% za kumfanya aweze kuwa mmiliki halali wa nyumba hizo na kufanya polisi wamkamate na kumuweka ndani ambapo alitoka baada ya siku kadhaa na kuanza kupata umaarufu mara dufu. 


Mkongwe aliye tamba enzi zake Mr.Nice afunguka haya

Msanii Mr. Nice ambaye siku nyingi amekuwa kimya kwa kutotoa kazi mpya, amejitapa na kusema kwamba kazi zake za mwanzo zilimpa faida kubwa na kuwekeza kiuchumi, kitendo ambacho kimemfanya aishi maisha ya raha sasa hivi.

Akipiga stori na Big Chawa wa Planet Bongo kwenye East Africa Radio, Mr. Nice amesema kutokana na fedha alizopata alijenga nyumba yake mwenyewe, na kwamba mpaka sasa yuko vizuri kiuchumi kani hata kufua hafui kwa mkono bali hutumia mashine, na hata akienda chooni habebi kopo na kusindikizwa na mbwa kama ilivyo kwa watu wengi wa kipato cha chini.

Monday, 20 November 2017

Peter ajiengua kuhusika na kuvunjika kwa kundi la P-Square


NYOTA wa muziki nchini Nigeria ambaye alikuwa anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa yeye si chanzo cha kundi hilo kuvunjika.

Kundi hilo kwa sasa limevunjika kwa madai kwamba kila mmoja alikuwa anafanya mambo kinyume na utaratibu na kila mmoja sasa anafanya kazi peke yake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapacha hao walikuwa wanasherehekea siku yao ya kuzaliwa, lakini kila mmoja alionesha kusherehekea kivyake japokuwa Paul aliposti picha yao ya utotoni.

Taarifa zilisambaa kwenye mitandao kwamba Peter ndio chanzo cha kuvunjika kwa kundi hilo, lakini ametumia ukurasa wake wa Instagram na kukanusha taarifa hiyo.

“Nashangaa kuonekana kuwa mimi ndio mwenye kosa, hakuna ukweli wowote nadhani kosa langu ni kuweka wazi tofauti zetu, ila mimi si chanzo kama watu wanavyosema kwenye mitandao ya kijamii, lakini nashukuru kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa,” aliandika Peter.

AT apongezwa na BASATA baada ya kunyakua ushindi wa tuzo Marekani

Baraza la Sanaa Taifa(BASATA)limempongeza msanii wa muziki AT kwa ushindi wa tuzo za Mama Awards zilizofanyika nchini Marekani wiki iliyopita.
AT alishinda tuzo mbili ambazo ni ‘International Artist’ na ‘Best Music Video’. Kupitia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Intagram wa baraza hilo imetoa pongezi kwa AT utokana na ushindi ailioupata na ubunifu.
Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya mduara nchini Ally Ramadhani maarufu kwa jina la kisanii “AT” ameshinda Tuzo mbili za MAMAWARDS huko nchini Marekani.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kama mlezi wa wasanii nchini linampongeza kwa dhati msanii “AT” pamoja na uongozi wake kwa heshima na sifa kubwa waliolipatia Taifa letu huko ughaibuni.
Aidha, BARAZA linapenda kuchukua nafasi hii kuwasihi wasanii nchini kuongeza ubunifu na ubora zaidi kwenye kazi zao ili sanaa yetu izidi kufika mbali zaidi kimataifa. #mamawards

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO 2019

https://youtu.be/3CLxlkAGSw0