Saturday, 18 November 2017

Ona maajabu ya rubani wa ndege hii

Rubani atumia ndege kuchora moja ya sehemu ya kiungo cha uzazi angani



Maafisa wa jeshi la wanamaji wamesema kwamba haikubaliki kwamba mmoja wa marubani wake alitumia ndege moja ya kijeshi kuchora uume wa mwanadamu angani.

Mchoro huo uliokuwa katika kaunti ya Okanogan magharibi wa jimbo la Washington nchini Marekani ulizua hisia nyingi katika mitandao ya kijamii.

Lakini makomando katika kituo hicho cha wanamaji kilichopo katika kisiwa cha Whidbey hawakuona ucheshi wake na sasa wameanzisha uchunguzi.

Msemaji wa kambi hiyo ya kijeshi alithibitisha kuwa ndege iliohusika kuchora uume huo kwa kutumia moshi wake ni ile ya Boeing EA-18G Growlers.

Ndege hiyo hutumika maalum kwa vita vya kielektroniki na inaweza kusafiri mara mbili kasi ya sauti.

Msemaji Thomas Mills aliambia BBC : Mimi kama mwanamaji tunawapatia heshima kubwa marubani wetu na hili halikubaliki hata kidogo.

Watazamaji waliokuwa chini ardhini walichekeshwa na mchoro huo.

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO 2019

https://youtu.be/3CLxlkAGSw0