Sunday, 19 November 2017

Zimbabwe hali ya zidi kuwatata kwa Mugabe wanajeshi na wananchi wamtaka aondoke madarakani

Zimbabwe hali ya zidi kuwatata kwa Mugabe wanajeshi na wananchi wamtaka aondoke madarakani

Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa mjini Harare wakijiandaa kwa mkutano mkubwa unaoungwa mkono na chama tawala ZANU-PF katika jitihada za kuongeza shinikizo la kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go.

Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.

Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.

Kikubwa kinachozozaniwa ni nani atakayemrithi rais Mugabe atakapoochia madaraka.

Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.

Mugabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.

Zaidi ya hayo Bw. Mugabe angependa kuendelea kuwa uongozini hadi chama kitakapofanya mkutano wao mkuu mwezi ujao. 

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO 2019

https://youtu.be/3CLxlkAGSw0