Monday, 20 November 2017

JE, WAJUA?

1. Je, wajua kwamba binadamu pamoja na akili zake zote, pamoja na mbwembwe zake nyingi, bado hana uwezo wa kufikisha ulimi kwenye kiwiko cha mkono wake?
2. Je, wajua kwamba kama piza zinazoliwa kwenye bara la Amerika kwa siku zingepangwa zingeweza kuchukua eneo lenye ukubwa wa hekta 18?
3. Je, wajua kwamba kila binadamu ana alama tofauti kabisa na za kipekee katika ulimi wake (tongue-prints) kama zilivyo za vidole?
4. Je, wajua kuwa mnyama aina ya mamba huwa hana uwezo wa kutoa ulimi wake nje kutokana na maumbile yake?
5. Je, wajua kuwa farasi na panya ndio wanyama pekee wasiotapika?
6. Je, wajua kuwa jicho la mbuni ni kubwa kuliko ubongo wake?
7. Je, wajua kuwa licha ya binadamu kuwa na uwezo wa kubana pumzi zake, bado hawezi kujiua kwa njia hiyo?
8. Je, wajua kwamba kwa wastani kichwa cha mwanadamu hubeba nywele zipatazo 100,000 na kila unywele unakua kwa wastani wa sentimita 12.5 kwa mwaka?
9. Je, wajua kuwa siafu ndio viumbe pekee wasiolala maisha yao yote?
10. Je, wajua kwamba mwanadamu ambaye anaweza kuishi kwa wastani wa miaka kati ya 50-60, anaweza kuzalisha kiasi cha mate kinachofikia galoni 10,000?
Je, wajua kuwa mwili wa mwanadamu una kiwango cha mafuta chenye kuweza kuzalisha miche saba ya sabuni?
11. Je, wajua kuwa katika ngozi ya mwanadamu mmoja pekee kuna idadi kubwa ya viumbe hai kuliko idadi ya wanadamu wote walioko katika ulimwengu mzima?
12. Je, wajua kuwa kama mdomo wako ukiwa mkavu kabisa huwezi kutofautisha ladha mbalimbali?
13. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu hutumia zaidi ya asilimia 25 ya oksijeni yote inayotumiwa na mwanadamu?
14. Je, wajua kuwa kila dakika moja inayopita, kuna seli kati ya alfu 30 hadi 40 zilizokufa zinazodondoka toka katika mwili wa mwanadamu?
15. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu umeumbwa kwa maji kwa kiwango cha asilimia 80?
16. Je, wajua kuwa kati ya viumbe wote duniani, ni mwanadamu pekee ambaye anaweza kulala kwa kutumia mgongo wake?
17. Je, wajua kuwa ukubwa wa jicho la mwanadamu daima ni ule ule toka anapozaliwa hadi anapozeeka? Pua na masikio hukua kwa kadiri mwanadamu anavyozidi kukua.
18. Je, wajua kuwa paka ana uwezo wa kubadili sauti yake na kufanya milio zaidi ya 100 tofauti tofauti wakati mbwa ana uwezo wa kufanya hivyo na kutoa sauti kumi tu?
19. Je, wajua kuwa visiwa vya Hawaii huvisogelea vile vya Japan kwa umbali wa inchi 4 kila mwaka?
20. Je, unajua kuwa kutengeneza karatasi mpya kutokana na karatasi za zamani zilizoisha matumizi yake kunaweza kusaidia kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia takriban 70 kulinganisha na kutengeneza karatasi hizo kutokana na miti?
Chanzo ::: Mitandao mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.

TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO 2019

https://youtu.be/3CLxlkAGSw0